Header Ads

NBC YAANDAA PATI NA WATEJA WAKE UZINDUZI WA KITENGO CHA PRIVATE BANKING SUITE

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu  akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo baada ya uzinduzi  wa kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha NBC  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kitengo hicho kipo katika  Jengo la Coco Plaza karibu ya ufukwe wa Coco Beach jijini humo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya  (kulia) akisalimiana na Meneja wa Tawi la NBC Sea Cliff, Mariam Kombo  katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya  (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Idara Huduma za Kibenki kwa Wateja  Wakubwa na Uwekezaji wa Benki ya NBC, Andre Potgieter katika hafla  iliyoandaliwa na benki hiyo baada ya uzinduzi wa kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu na wa pili kulia ni mteja wa benki hiyo, Paul Chizi.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa  cha NBC, Andrew Massawe akizungumza katika hafla hiyo. Pamoja naye ni  baadhi ya maofisa katika kitengo hicho cha wateja binafsi wakubwa.
Mmoja wa wateja wa NBC, Paul Chizi akiipongeza Benki ya NBC kwa jitihada za kuanzisha kitengo maalumu cha kuhudumia wateja wakubwa (Private Banking).
Wasanii wa kikundi cha sarakasi cha Mama Afrika wakitoa burudani  katika hafla hiyo.

No comments

Powered by Blogger.