Header Ads

MBUNGE SHABIBY ATOA UDHAMINI WA KIKUNDI CHA WAANDISHI WA HABARI WAJASIRIAMALI (HABARI GROUP).!


MBUNGE wa jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby ambaye ni mmiliki wa kampuni ya mabasi, Shabiby Line Bus Services, ametoa udhamini kwa kikundi cha Waandishi wa Habari Wajasiriamali (Habari Group), watakaotembelea bunge mjini Dodoma wiki hii.

Habari Group wamepata mwaliko wa kutembelea Bunge, kutoka kwa Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki. Angellah pia ni mlezi wa kikundi hicho, ambapo pamoja na mambo mengine, Habari Group watakuwa na mkutano na mlezi huyo  na wadau mbalimbali wakiwemo wabunge kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya kikundi.

Akizungumzia udhamini huo, Shabiby alisema ameguswa na malengo ya
kikundi hicho, na kuamua kukisaidia kama mchango wake kwa maendeleo ya taifa .Alisema, kwa kuwa kampuni yake ni ya kizalendo, kusaidia makundi kama Habari Group ni moja ya majukumu ya Shabiby Line.

Mwenyekiti wa Habari Group, Mwanamkasi Jumbe, alishukuru kwa udhamini huo, ambao unahusisha usafiri na kwamba inawapa moyo kuona viongozi na wafanyabiashara mbalimbali kuunga mkono juhudi za wasichana, hasa wenye malengo ya kujikomboa.

Alisema waandishi wa habari wengi wamekuwa hawana malengo, na mwisho wa siku kuishia pabaya, lakini wameamua kujikusanya na kuweka akiba zao kwa manufaa ya baadaye.

Alimsifu Angellah, ambaye amekuwa akijitolea kwa kiasi kikubwa
kuhakikisha kikundi hicho kinasonga mbele, na kuomba wadau mbalimbali kujitokea na kusaidia makundi kama hayo.

No comments

Powered by Blogger.