Header Ads

MAN UNITED ILICHEMSHA DAU LANGU- KHEDIRA

NYOTA wa Real Madrid, Sami Khedira amesema Manchester United ilitoa ofa ya Pauni Milioni 34 kumsajili kabla ya dirisha ya usajili kufungwa jana.
 
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani alikuwa kwenye rada za kocha David Moyes wa United, lakini wakashindwa kumnasa kiungo huyo kabla ya saa 5:00 usiku.
Madrid ilijiandaa kuuza wachezaji ili kufidia gharama ilizotumia kumsajili Gareth Bale Pauni Milioni 86, lakini Khedira amesema dili lake lilikwama.
United target: Khedira has revealed that David Moyes made a late bid to secure his services
United walimtaka: Khedira amesema David Moyes alitoa ya kumsajili dakika za lala salama
"Klabu ilikataa pfa hiyo na ndivyo ilivyokuwa,"alisema Khedira kuwaambia Waandishi wa Habari mkutanoni mjini Munich.
"Hatukupata nafasi haswa ya kujadili hili. nilikuwa nina mawasiliano ya muda mrefu na Carlo Ancelotti wiki chache zilizopita na hiyo ndiyo sababu haswa ya mimi kubaki Real."alisema.
Press conference: Khedira addresses the media while on international duty for Germany on Tuesday
Mkutano na Waandishi wa Habari: Khedira akizungumza na Waandishi wa Habari 
International: Khedira has made 40 appearances for Germany
Wa kimataifa: Khedira ameiochezea mechi 40 Ujerumani

No comments

Powered by Blogger.