Header Ads

IANPHI KUFANYA MKUTANO WAKE WA 8 TANZANIA

 Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI), Tanzania imepewa heshima ya kuratibu mkutano wa nane wa mwaka wa  taasisi hiyo  na kupata nafasi ya kuing'arisha nchi katika ramani ya dunia na hatimaye kuweza kutangaza maliasili zake na vivutio vya Utalii vilivyomo. Mkutano huo wa nane wa IANPHI unataraji kufanyika kuanzia 29 Septemba 2013 hadi 1 Oktoba mwaka huu jijini Arusha katika Hoteli ya Ngurdoto.
 Akizungumza hii leo jijinni Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Chama cha Kimataifa cha Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii(IANPHI) na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dr. Mwele Malecelaamesema mkutano huo utashirikisha washiriki 150 kutoka nchi 73 wanachama.

 Daktari. Mwelecele Malecela ameimabia Father Kidevu Blog, katika ofisi zake za NIMR jijini Dar es Salaam hii leo kuwa mkutano huo unataraji kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Daktari. Hussein Mwinyi.
Makamu huyo wa Rais wa IANPHI Daktari. Mwele amesema kuwa wanachama wa taasisi hiyo watakao shiriki katika mkutano huo hususan wakuu wa Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii watapa fursa ya kujadili masuala muhimu ya afya ya jamii: kugbadilishana uzoefu na kubuni mbinu za kitaalam za kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya afya ya jamii.

"Mkutano pia utatoa nafasi kwa washiriki kujadili mbinu za kukuza ushirikiano ili kuimarisha afya ya jamii kuelekea mwaka 2015, ambapo mataifa yamejiwekea nia ya kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG's).

Kauli mbiu katika mkutano huo wa mwaka 2013 ni "Afya ya Jamii baada ya mwaka 2015 na mabadiliko ya majukumu ya Taasisi za kitaifa za afya ya Jamii" 

Chama hicho cha IANPHI kina wanachama 81 huku makao makuu ya Sekretarieti yake yakiwa mji wa Helsinki, Finland.

No comments

Powered by Blogger.