Header Ads

HATIMAYE KAZI KWISHA, BALE AJIUNGA REAL MADRID, AIPIKU REKODI YA RONALDO, KUPIMWA AFYA LEO!!

HATIMAYE  Gareth Bale amekamilisha uhamisho wake jana usiku kujiunga na Real Madrid kwa dau nono la pauni milioni 86 na kuvunja rekodi ya pauni milioni 80 ya Cristiano Ronaldo wakati ule akiunga na klabu hiyo  mwaka 2009.
 
Baada ya makubaliano, Bale atalipwa pauni laki 2 na elfu 56 kwa wiki, na ameanguka mkataba wa miaka 6 na leo hii jumatatu anatarajiwa kupima afya yake tayari kwa kazi moja ya kuing`arisha Real Madrid na kutambulishwa kwa waandishi wa habari.

Sasa Bale amekuwa mchezaji ghali zaidi duniani baada ya kupiku rekodi ya Ronaldo, na kilichobaki kwake ni kuonesha kuwa ana uwezo mkubwa na analingana na dau kubwa kiasi hicho.

He's here: Real Madrid's new recruit Gareth Bale poses with fans after arriving at Barajas Airport 
Yuko hapa: Nyota mpya wa Real Madrid, Gareth Bale akiwa katika pozi la picha na mashabiki baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Barajas 
On the move: Gareth Bale, out in London on Saturday, has finally completed his move to Real Madrid 
Akiondoka: Gareth Bale, wakati akiondoka  London jumamosi na hatimaye amekamilisha usajili wake kujiunga na miamba ya Hispania,  Real Madrid
Final shot: Bale is leaving Tottenham after featuring in just one pre-season friendly this campaign 
Mara mwisho: Bale ameondoka Tottenham akiwa amecheza mechi moja tu ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England

No comments

Powered by Blogger.