Header Ads

DKT SHEIN;ZANZIBAR IMECHANGIA SANA KUKUZA NA KUENEZA USTAARABU MAENEO YA AFRIKA MASHARIKI.

NA RAMADHANI ALI/HABARI MAELEZO ZANZIBAR   
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Dkt. Ali Muhammed Shein amesema Historia inaonyesha kuwa Zanzibar imechangia sana katika kukuza na kueneza ustaarabu wa kiislamu katika maeneo ya Afrika Mashariki.
Amesema Masheikh na Maulamaa wa Zanzibar  walikwenda kueneza Uislamu katika maeneo  ya Ukanda huo na wengine walifika visiwa vya Comoro  na nchi nyengine za Afrika ya Kaskazini na baadhi ya nchi za Asia.
Dkt. Shein ameeleza hayo alipokuwa akifungua Kongamano la Kimataifa kuhusu Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu katika nch za  Afrika Mashariki linalofanyika katika Hoteli ya Lagema, Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema anaamini kuwa kutokana na Historia  na vigenzo  vyengine vingi ndio viliopelekea  Mamlaka ya Kumbukumbu na Nyaraka ya Falme  ya Oman kuichagua Zanzibar kuwa mwenyeji wa kongamano hilo la Kimataifa la kiislamu kwa nchi za Afrika Mashariki.
“Kwa hakika Zanzibar ndiyo kitovu cha Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu katika nchi za Afrika Mashariki, hivyo kuichagua Zanzibar kuwa mwenyeji wa kongamano hili ni pahala pake,”alisisitiza Dkt. Ali Muhammed Shein.
Amongeza kuwa yapo maelezo ya kihistoria yanayoeleza kwamba msafara wa viongozi wa dini ya kiislamu ukiongozwa na Sayyid Jaffar bin Abu Talib waliingia Zanzibar na kufikia kijiji cha Ndagoni Pemba kabla ya viongozi wengine wa dini kuingia Madina.
Amesema  lugha ya Kiswahili imekuwa chombo muhimu cha   kueneza na kuendeleza ustaarabu na mafundisho mengine ya dini ya kiislamu kupitia mawaidha, darsana pia tafsiri za vitabu vya dini ya  kiislamu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

No comments

Powered by Blogger.