Header Ads

DK ALBERIC KACOU AFUNGUA WARSHA KWA WARATIBU WAKAZI MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA JIJINI DAR LEO


IMG_5252
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akifungua warsha siku tano kwa Waratibu Wakazi wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika inayosisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kwenye shughuli na majukumu ya Umoja wa Mataifa katika za Kusini mwa Afrika yenye ujumbe wa Delivering As One (DAO) kutoa matokeo ya pamoja katika kuratibisha na kuboresha majukumu ya Umoja wa Mataifa katika nchini hizo.

Akifungua warsha hiyo Dk. Kacou amesisitiza umuhimu wa mkutano kuwapa jukwaa wafanyakazi wote wa Ofisi za waratibu wakazi jinsi ya kujielimisha na kupata habari ya mabadiliko ya Dunia na majukumu ya Kikanda yanayoendana na maboresho ya kuratibu shughuli za Umoja wa Mataifa wenye lengo la kuleta matokeo ya pamoja.

Alisema warsha hiyo itawajengea uwezo kwa washiriki umuhimu wa kujenga mazoea ya kujielimisha kimkakati na stadi za kazi zenye kuleta ufanisi katika kusaidia kuleta mabadiliko ya kazi za Umoja wa Mataifa katika nchi za Kusini mwa Afrika.

Dk. Kacou ameongeza katika kuleta matokeo ya pamoja Waratibu wakazi wanajukumu la kuhakikisha Haki za Binadamu na Mashirika yanayotetea Haki za Binadamu yanapewa wigo mpana katika kushiriki kwenye mchakato wa Demokrasia na Haki za Binadamu.

Amefafanua kuwa Mkutano huu unafanyika Tanzania kwa sababu ni nchi iliyoonyesha mafanikio katika nyanja hizi za Kiuchumi, Kisiasa, Demokrasia na Haki za Binadamu.

Warsha hiyo iliyoandaliwa na Kikundi cha Kikanda cha Maendeleo Umoja wa Mataifa (UNDG) Mashariki na Kusini mwa Afrika ambayo ilikuwa na kauli mbiu ya kuchukua na kupeleka mbele mabadiliko ya kimkakati yanayoleta matokeo ya pamoja.
IMG_5294
Kamishina Msaidizi wa Bajeti Wizara ya Fedha Bw. Jerome Buretta akizungumza kwenye majadiliano ya warsha hiyo kwamba Serikali ya Tanzania iliamua kuingia katika mpango huu wa matokeo ya pamoja(DAO) na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ili kuleta ufanisi katika nyanja mbalimbali ambazo zinafadhiliwa na Umoja wa Mataifa hapa nchini.

Bw. Buretta amesema katika mpango huo inaiwezesha Serikali kukaa pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa na kupanga Bajeti na matumizi ya fedha zitolewazo na nchi wahisani ili kuhakikisha inaleta matokeo chanya kwenye jamii.
IMG_5266
Baadhi ya Maofisa kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku tano iliyoanza leo jijini Dar.
IMG_5304
Kwa upande wake Kansela wa Mambo ya Siasa Ubalozi wa Norway nchini Bi Elisabeth Schwabe Hansen amesema kwamba nchi yake ya Norway ni mdau wa muda mrefu wa maendeleo nchini Tanzania katika kuhakikisha maboresho na mipango ya Umoja wa Mataifa yanapitia katika mkondo sahihi kuhakikisha miradi ya maendeleo na ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Tanzania unaleta matokeo ya pamoja.
Bi. Hansen ameongeza kuwa katika mipango hiyo ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania ni kuhakikisha inajenga uwezo wa rasilimali watu na kuratibu programu za Umoja wa Mataifa ambazo zinaendana na dira ya maendeleo ya Taifa.
IMG_5333
Mmoja wa Afisa kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akibadilishana uzoefu juu ya Programu hii ya matokeo ya pamoja kwa baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.

No comments

Powered by Blogger.