Header Ads

AIRTEL TANZANIA YAMTEUA MKURUGENZI MPYA WA KITENGO CHA TEKNOLOJIA IT.Airtel Tanzania inatangaza uteuzi wa Bw. Frank Filman kuwa mkurugenzi
wa kitengo cha teknolojia ya IT aliyechukua nafasi hiyo rasmi kuanzia
sasa

Filman ambaye ni mtanzania alianza kazi Airtel akiwa kama munagalizi
wa system (system Admistrator) na baadaye alipanda cheo na kuwa Meneja
wa Mradi wa Technolojia ya IT. Kutoka mwaka 2007 mpaka 2009, alikuwa
Meneja wa kitengo hicho nchini Ghana ambapo alisimamia na kutoa
mchango mkubwa  uzinduzi wa mtandao wa Airtel  nchini Ghana.

Mwishoni mwa mwaka 2009 Filman alirejea Tanzania akiwa kama Meneja wa
Huduma za kimtandao  (Network service Manager ) za Airtel Tanzania.

Baadaye alijiunga na kitengo cha mauzo na kama meneja wa Techonologia
na biashara na huko aliweza kuchangia ongezeko la mapato kwa kiasi
kikubwa hadi kufikia 100%  kwa mienzi 12 tu.

Katika miaka yake 12 na Airtel, Filman amefanya kazi miaka miwili
Airtel Ghana na zaidi ya miaka tisa akiwa na Airtel Tanzania.

Akizungumzia juu ya uteuzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa Airtel
Tanzania, Sunil Colaso alisema "Uteuzi wa Filman kuwa Mkurugenzi wa
kitengo cha Teknolojia ya IT ni ushahidi wa dhamira ya Airtel Tanzania
kuendeleza, kulea na kukuza vipaji vya wafanyakazi wake ndani ya nchi.
Sisi tunayo furaha kubwa kuona Watanzania wanachukua majukumu makubwa
katika moja ya makampuni yanayokuwa kwa kasi na nyeti kama
hii.Teknolojia ya IT ni msingi muhimu wa mafanikio katika mawasiliano
ya simu kwa sababu huduma zetu mbalimbali ikiwa ni pamoja na  huduma
za kifedha yaani Airtel Money na  internet zinategemea teknolojia
hiyo."

Aliendelea kwa kusema Kampuni imemteua Bw. Filman ikiwa na uhakika
kwamba ataifanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa kabisa.

"Tunaamini Bw. Filman atafanya vyema kazi yake kutokana na uzoefu
alionao lakini vilevile Airtel itaendeleza dhamira yake kuwaendeleza
na kuwawezesha wafanyakazi wengine kushika nyazifa kama hizi nchini na
kwenye nchi nyingine za Afrika na Asia ambapo Airtel inafanya
biashara. pia Airtel tutaendelea kuwapa mafunzo wafanyakazi wetu
ambayo yatawafanya wawe kwenye viwango vya kimataifa" Alisema Bw.
Golaso.

Akizungumzia uteuzi wake Filman alisema, "Nimekuwa nikitamani kupata
nafasi hii na nilijua siku moja naweza nikaipata na ninayofuraha
kupata wadhifa huu Airtel Tanzania . kwa miaka mingi nimepitia mafunzo
mbalimbali, na nina uzoefu nilioupata nchini Ghana pamoja na nchi
nyingine Airtel inayofanya biashara. Hivyo niko tayari na nimejiandaa
vyema kukabiliana na changamoto zote katika utendaji wa kazi hii na
kuhakikisha natoa huduma zenye ubora kwa watanzania."

Airtel tunamini wafanyakazi ndio nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko
ya kitamaduni , kasi ya kazi na kibiashara.  Airtel imewekeza katika
kukuza uwezo wa wafanyakazi na kutoa nafasi ya kukuza fani ndani ya
kampuni. Mafunzo ya ujuzi daima imekuwa ni mikakati yetu inayoendana
sambamba na ujuzi unaohitajika kimataifa alisema bw Sunil Colaso
mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania

Airtel imeweza kutoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wake ili
kuhakikisha wafanyakazi wa Airtel wanatoa huduma bora za kitaalamu kwa
Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kumekuwa na fursa ambazo zimekuwa
zikitolewa kwa wafanyakazi wa Airtel Tanzania katika vitengo vya
masoko, Mauzo, IT, pamoja na kuwa na mfumo wa kuwapeleka baadhi ya
wafanyakazi wake nchi tofauti kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwa
kufanya kazi kwa mienzi 6 hadi 18 katika Airtel Afrika na India.


Airtel pia imekuwa ikiendesha mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wa
mauzo, masoko na huduma kwa Wateja kupitia Chuo Kikuu cha Centum .
Ambapo wafanyakazi wamekuwa wakipewa ujuzi na maarifa muhimu
yanayowasaidia kutoa huduma bora kwa wateja ambazo zinaleta maendeleo
makubwa na kuonesha utofauti katika soko la ushindani la mawasiliano
ya simu.

No comments

Powered by Blogger.