Header Ads

Snura atajwa kwenye list ya Serengeti Fiesta Mtwara

Wasanii maarufu wa kizazi kipya zaidi ya Kumi tano watatoa burudani kwa mara ya kwanza kwa wakazi
wa mkoa wa Mtwara na majirani zake katika tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2013 ambalo ni maarufu
kwa ”Tupo Pamoja, Twenzetu, Tukawinde” Ni Noma sanaa” litalofanyika katika uwanja wa Nangwanda
uliopo mjini Mtwara. Burudani hiyo itakuwa kivutio tosha kwa wakazi wengi kutokana na kundi kubwa la
wanamuziki wa kizazi kipya waliopo kwenye chati za juu katika muziki huo.

Tamasha hilo linaambatana na shamrashamra zinazoendelea kwenye promosheni za bar mjini hapo
ambapo wakazi wa Mtwara watakuwa wakijishindia tiketi za bure pamoja na fulana baada ya kujibu
maswali marahisi, pia kutakuwa na washindi ambao watapata nafasi ya kuwakilisha Mtwara kwenye
tamasha la kuhitimisha msimu wa Fiesta 2013 jijini Dar Es Salaam. 

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa tamasha hilo kubwa la kila mwaka, Msanii mkali katika miondoko ya kipwani Snura(Pichani juu), ambaye ni maarufu kwa wimbo wake wa ”Majanga” ataungana na wasanii wengine waliofanya vizuri kwenye tamasha hilo lililoanzia mkoani Kigoma ambapo ilikuwa kwa mara ya kwanza pia, ikafuatiwa na Tabora na Singida wikiendi iliyopita.

Wasanii zaidi ya kumi na tano wanaokubalika kama Nay wa Mitego, Makomandoo, Juma Nature, Matonya, Kassim Mganga,  Chege na Temba, Snura, Madee, Young Killer, Stamina, Godzilla, Nikki Wa Pili, Ommy Dimpoz na Pasha ambaye anatokea mkoani Mtwara watapanda jukwaani kukonga nyoyo za wakazi wa mji wa Mtwara siku ya Jumamosi.

No comments

Powered by Blogger.