Header Ads

SIENDI POPOTE...HII NDIO KAULI YA FABREGAS ALIYO ITOA LEO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI


HATIMAE Cesc Fabregas amekata mzizi wa fitina kwa kumaliza uvumi kuhusu uwezekano wa yeye kwenda Manchester United akiongea hii leo mbele ya waandishi wa habari Cesc amesisitiza kuwa ana 'furaha sana' kuwepo Barcelona.

Kocha wa United David Moyes alipeleka ofa mbili kwa ajili ya mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal ambazo zote zilipigwa chini na Barcelona mapema katika majira haya ya kiangazi,huku  mkurugenzi wa michezo wa mabingwa hao wa Hispania, Andoni Zubizarreta akitangaza mwanzoni mwa wiki hii kuwa United imenyanyua mikono katika jitihada zao za kutaka kumsaini kiungo huyo wa Hispania.

Lakini akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari hii leo , kiungo huyo alisema: 'kushinda ndani ya Barcelona ni kitu ambacho nimekuwa na matumaini nacho kwa muda mrefu katika maisha yangu yote , imekuwa ni ndoto yangu tangu nikiwa mtoto.
'Nina furaha sana kuwa Barcelona na sijawahi zungumza na klabu nyingine yoyote katika miaka miwili iliyopita.'

Fabregas pia alijitetea kuwa hajawahi toa taarifa juu ya mustakabali wake wakati wa kipindi chote cha uvumi kuhusu yeye kwenda United.

Nilikuwa nimetulia sikuwa na wasiwasi kabisa kuhusu hilo katika kipindi chote hicho, Sikuwa na haja ya kufafanua kuhusu chochote kwa kuwa kitu pekee nilichokuwa nawaza ni kuhusu kubakia Barcelona,alisema.
Kama ambavyo sikumdanganya yeyote au kuficha chochote, niliwaambia waandishi wa habari wa klabu kuwa nitazungumza siku zamu yangu ya kuongea kwenye mkutano na vyombo vya habari itakapofika.

Na alisisitiza kuwa hakukuwa na ukweli wowote katika uvumi kuhusu yeye kutaka kurudi Ligi Kuu ya uingereza.

Hadithi kuhusu yeye zimekuwa ni za kutunga,alisema. sijui ni kwa nini uvumi huu uliendelea kukua hata baada ya Tito (Vilanova,kocha wa zamani wa Barca), Zubizarreta, Tata (Gerardo Martino, kocha mpya wa Barca ) na (Makamu wa rais wa Barca,Josep) Bartomeu wote kusema wanataka nibaki.

'Kamwe sikupewa ishara yoyote kutoka klabuni ya kufanya mimi nadhani kuwa hawaniitaji,daima nilijiskia kuwa nahitajika hapa.

Mimi binafsi niliongea na Bartomeu, rais (Sandro Rosell) na Tata pia aliniambia anahitaji nibakie na hakuna tatizo.'

Fabregas pia alikana kuwa eti aliomba mkataba mpya kutoka Barca na kuahidi kuboresha kiwango chake kwa ajili ya msimu ujao.

'Nachotakiwa kufanya ni kufanya kila kitu vizuri kwa sababu nipo katika klabu kubwa na yenye hadhi duniani,"alisema.

No comments

Powered by Blogger.