Header Ads

SHULE YA MSINGI KUMBUKUMBU YAKABIDHIWA MRADI WA MAJI


DSC_1479
Rais wa Rottary Club Mzizima, Ambrose Nshala na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge wakikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji uliofadhiliwa na klabu hiyo katika shule ya msingi Kumbukumbu Dar es Salaam jana.
DSC_1457Rais wa Rottary Club Mzizima, Ambrose Nshala (kushoto), akijadiliana jambo na Naibu Meya Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge na Diwani wa Kata ya Kinondoni, Husna Hemedi wakati wa hafla ya kukabidhi mradi wa kisima cha maji uliofanyika Dar es Salaam jana.

 
………………………………………………………………..
 
 Shule ya Msingi Kumbukumbu iliyopo katika Manispaa ya Kinondoni jana ilikabidhiwa mradi wa maji safi ya kunywa  wenye thamani ya zaidi ya Sh15Milioni uliotekelezwa na Klabu ya Rottary Mzizima.
 
Akizungumza mara baada ya kupokea mradi huo kutoka kwa Rais wa klabu hiyo, Ambrose Nshala katika hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo jana, Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge alisema mradi huo una umuhimu wa pekee kwa kuwa shule nyingi za Dar es Salaam hazina huduma za maji.

Alisema kutokana na hali hiyo wanafunzi wengi wamekuwa wakienda shuleni na vidumu vya maji kwa ajili ya matumizi ya vyooni kwa wanafunzi na hata walimu jambo ambalo linahatarisha afya zao kwani maji ya namna hiyo ni machache na yasiyokidhi mahitaji.
 
Songoro alisema mradi huo umewapata changamoto kwao kutokana na ukweli kuwa kiasi cha fedha kilichotumika ni kidogo kulinganisha na mradi wenyewe na kiwango hicho kisingewezekana kwa miradi inayotekelezwa na manispaa na mradi kama huo ungeweza kugharimu hadi Sh100 Milioni.
 
“Sheria ya manunuzi ni tatizo kwani kwa mradi huu ungeambiwa si chini ya Sh100Milioni zimetumika na hilo ni tatizo ambalo linakwamisha utekelezaji wa miradi mingi katika manispaa” alisema na kuongeza kuwa kuna miradi mingi utekelezaji wake umekwama kutokana na watalaam kuwasilisha bajeti zisizowezekana.

Awali akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo, Rais wa Rottary,  Ambrose Nshala  alisema mradi huo ambao unahusisha matenki ya maji ya lita zaidi ya 10,000 una mashine pia ya kusafisha maji na kuyafanya yawe salama kwa kunywa kwa watoto moja kwa moja kutoka bombani.

Alisema mradi huo ni fedha zao wanachama na wahisani wengine na zingine zimetokana na mbio za hisani za Rottary Marathon na shule hiyo ni moja kati ya zingine 25 za Jijini Dar es Salaama ambazo zimesaidiwa kutatua kero mbalimbali na wahisani hao.

No comments

Powered by Blogger.