Header Ads

SBL YAUNGA MKONO KILIMO KWANZA

 Meneja kilimo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Shafii Mndeme akitoa ufafanuzi kwa wakulima juu ya changamoto wanazozikabili na namna Kampuni ya Bia ya Serengeti itakavyozitatua kero hizo wakati
alipotembelea mashamba ya wakulima hao Basutu wilayani Hanang katika mkoa wa  Manyara. Ufafanuzi huo ulitolewa baada ya kampuni ya bia ya Sereengeti kutembelea wakulima wa shayiri katika kana ya kaskazini.

 Wakulima wa shayiri katika kata ya Ngare Nairobi mkoani Kilimanjaro, wakikagua shayiri ya mkulima mwenzao ambaye alipata mbegu kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kampuni hiyo iliwatembelea wakulima hao wa kanda ya kaskazini na  kujadili jinsi ya kukuza kilimo cha zao hilo huku kampuni hiyo ikitatua matatizo yanayowakabili wakulima hao kwa kuwapatia pembejeo na kuwaahidi  kuwaletea mtaalam wa kupima udongo ili kujua ni mbolea gani thabiti  itumike ili kupata mavuno yanayoridhisha.
 Diwani wa kata ya Ngare Nairobi wilayani Siha,  mkoa wa Kilimanjaro akitoa maelekezo kwa wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ambao ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Imani Lwinga(wa pili kushoto) pamoja na Meneja kilimo wa kampuni hiyo Shafii Mndeme(wapili kulia) wakati walipotembelea mashamba ya shayiri katika kata hiyo kwa lengo la kuwainua wakulima.
Menaja mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Imani Lwinga(kushoto) pamoja na Meneja kilimo wa kampuni hiyo Shafii Mndeme(kulia) wakikagua shayiri katika shamba la Bora Msaki mmoja wa
wakulima wanaonufaika na mradi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti mkoani Kilimanjaro katika kata ya Ngare Nairobi wilayani Siha. Kampuni hiyo inaunga mkono kampeni ya Kilimo Kwanza kwa kuwapa mbegu na kuwahakikishia soko la kuridhisha wakulima wa shayiri kanda ya kaskazini.KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAENDELEZA SERA YA KILIMO KWANZA
*Yawaunga mkono wakulima wa shayiri na ngano mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.Na Mwandishi Wetu
Wakulima wa kanda ya kaskazini katika mikoa ya  Arusha, Kilimanjaro na Manyara wamenufaika kupitia kampuni ya bia ya Serengeti  baada ya kampuni hiyo kuwapatia pembejeo bora na za kisasa pamoja na kuwahakikishia soko la uhakika kwa ajili ya bidhaa zao kwa kununua mazao yao kwa bei yenye kukidhi mahitaji ya wakulima hao. Hayo yalibainishwa baada ya kampuni hiyo kuwatembelea wakulima hao na  kujadili changamoto, fursa na mikakati mbalimbali ya wakulima hao.

Wakulima hao wakiwa na furaha kubwa walibainisha kuwa kampuni ya bia ya Serengeti imekuwa ni mkombozi mkubwa sana kwao kwani kampuni hiyo imekuwa na ahadi za kweli kwa wakulima hao kwa kuwapatia mbegu za kisasa, kuwalipa kwa wakati na kikubwa zaidi kuwajali kwani suala la kuwatembelea na kujadiliana nao juu ya changamoto zinazowakabili na kutoa suluhisho la matatizo hayo ni ushahidi tosha kwamba kampuni ya bia ya Serengeti inawajali wakulima na kuonesha kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza  kaulimbiu ya kilimo kwanza nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Kampuni ya Bia ya Serengeti, Meneja kilimo wa kampuni hiyo Shafii Mndeme alisema, “Hadi kufikia mwaka 2017 tunahitaji Tani 30,000 za shayiri na mpaka sasa tumepata tani 3000 tu za zao hili la shayiri, uhitaji bado ni mkubwa sana. Wito wangu kwa wakulima ni kujikita katika zao hili kwa kufuata maelekezo ya kilimo cha kisasa na kuotesha mbegu kwa wakati. 

Katika kuunga mkono  juhudi za serikali yetu ya Tanzania katika sera ya kilimo kwanza, tunahitaji wakulima zaidi ya 100 na kwa sasa tumeanza na wakulima wa zao la shayiri katika mikoa ya kaskazini na mtama mweupe kwa mikoa ya kanda ya kati kwa kuwapa pembejeo za kilimo na soko la uhakika kwa mazao yao. Tunampango wa kuanzisha bidhaa inayotokana na zao la muhogo hivyo mkoa wa Mtwara na Mbeya wakae mkao wa kula”.

Kampuni ya bia ya Serengeti inajivunia kutumia malighafi za hapa  nchini kuzalisha vinywaji vyake. Pia kampuni hiyo inatumia malighafi za Tanzania katika viwanda vyake nchini Kenya na Uganda hivyo kupanua wigo wa soko la shayiri Afrika Mashariki.  Bwana Mndeme alitoa wito kwa serikali kuwa Serikali ipunguze ushuru kwa wakulima wanapopeleka mazao yao sokoni ili kuwafanya wakulima waweze kunufaika na kilimo kwa kupata mapato yatakayokidhi mahitaji yao. 

Pia serikali izifikirie kampuni mbalimbali nchini zinazowasaidia wakulima na kuwapunguzia kodi ili waweze kusaidia wakulima wengi zaidi nchini.
Naye diwani wa kata ya Ngare Nairobi wilayani Siha, Daniel Sandawa ambaye pia ni mkulima wa zao la shayiri Magharibi mwa mkoa wa Kilimanjaro alisema, “kwa niaba ya wakulima wa Ngare Nairobi tunaipongeza sana Kampuni ya bia ya Serengeti kwa ushirikiano na msaada mkubwa wanaotupatia katika kuendeleza kilimo cha shayiri. Kwani mkulima anapopeleka shayiri sokoni hulipwa ndani ya siku 14 kwa bei ya Tsh. 850 kwa kilo  ambapo awali haikuwa hivo kwa kampuni zingine tulizowahi kufanya nazo kazi”.

Akiongea kutoka mashamba ya Basutu wilayani Hanang mkoani Manyara, Emannuel Hhawu Axwesso ambae pia ananufaika na mradi huu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, “tulikata tamaa kulima zao hili la shayiri kwani wakulima wadogo walikuwa wakinyanyasika katika swala la mgawanyo wa pembejeo na bei sokoni wakati wa kuuza mazao yetu.

Tunaipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kujali wakulima wa aina zote bila kujali kuwa ni mkulima mdogo au mkubwa. Hii inatupa moyo wakuendelea kulima zao hili na tunaahidi kuongeza uzalishaji wa shayiri endapo changamoto tulizonazo zikitatuliwa.Tunahitaji vifaa vya kisasa zaidi, utafiti wa kina wa aina ya udongo katika mazingira yetu ili kujua ni aina gani ya mbolea inaweza kutuletea mazao mengi zaidi ”.

Changamoto hizo za wakulima zilijibiwa na Meneja kilimo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti bwana Mndeme, ambapo alisema mwanzoni mwa mwezi Septemba wataalamu wa kilimo kutoka `International Crop Care’ kutoka nchini Kenya watakuja kufanya utafiti katia maeneo ya Kilimanjaro Magharibi na tayari wameshaingia mkataba na wakala wa mbolea ambayo itapendekezwa na wataalam hao.

No comments

Powered by Blogger.