Header Ads

RODGERS: “LIVERPOOL NDIO WENYE MAMLAKA, HATUMUUZI SUAREZ, AKITAMBUA HILO ATARUDI KATIKA KIWANGO BORA”!!

Kocha Brendan Rodgers amesema Liverpool ina mamlaka yote ya kuamua maisha ya baadaye ya Luis Suarez na nyota huyo atafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita baada ya kugundua kuwa haruhusiwi kundoka.
 
Arsenal bado wanaendelea kumshawishi Suarez ambaye msimu uliopita alikuwa mhimili wa Liverpool, na wanatarajia kuongeza dau kubwa zaidi ya pauni milioni 41 walizotuma awali na kukataliwa.

Arsene Wenger mapema jana alithibitisha kuwa ana matumaini ya kumsajili mshambuliaji huyo, lakini Rodgers alimuamuru  Saurez kufanya mazoezi peke yake baada ya kurudia kauli yake ya kutaka kuondoka, ila amesema anaamnini atabakia Anfield.

‘Sisi tumetulia’ alisema Rodgers. ‘ Klabu ndiyo yenye mamlaka juu ya suala hilo. Mmiliki wa timu anajua hilo na ana akili sana, amekaa kimya na ameweka wazi na kutuunga mkono kuwa tunahitaji kuwa naye msimu ujao.

Driving force: Luis Suarez, pictured leaving training on Friday, is ready to quit Liverpool 
Akiendesha mkoko wake: Luis Suarez, alipigwa picha akiondoka na gari lake katika mazoezi ya jana na yupo tayari kuondoka Liverpol.
Relaxed: Brendan Rodgers believes Liverpool are 'in control' of Luis Suarez's future 
Ametulia: Brendan Rodgers anaamini Liverpool ndio wenye mamlaka juu ya hatima ya baadaye ya Luis Suarez
Controversial: Luis Suarez's bid to leave Liverpool has dominated the summer 
Haeleweki: Dili la Luis Suarez kutaka kuihama Liverpool majira haya ya kiangazi limedhibitiwa na mabosi wake

No comments

Powered by Blogger.