Header Ads

NI VIGUMU KUBAINI JERAHA CHINI YA MKONO WA KULIA ALILILOPATA KATIBU WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA SHEIKH ISSA PONDA LIMESABABISHWA NA KITU GANI - MOI

 Sehemu ya kodonda katika bega la Sheikh Ponda baada ya kushinwa nyuzi.
  Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, akiwa katika Wodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akitibia jeraha alilopata jana akidaiwa kupigwa risasi mjini Morogoro.
 Sheikh Ponda akiwa hospitalini hapo na jeraha katika bega la mkono wa kulia.
Sheikh Ponda akiwa na msaidizi wake hospitalini hapo.
******************************************************
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu – MOI imesema imekuwa ni vigumu kubaini jeraha chini ya mkono wa kulia alililopata Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh ISSA PONDA limesababishwa na kitu gani.
 
Akizungumza na waandishi kuhusiana na majeraha ya Sheikh PONDA Afisa Habari wa Taasisi hiyo JUMAA ALMASI amesema ugumu wa kutokubaini sababu za jeraha hilo unatokana na tiba ya awali aliyopatiwa ikiwa ni pamoja na kushonwa jeraha hilo kabla ya kufikishwa - MOI.
 
ALMASI amebainisha kuwa baada ya Katibu huyo wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu nchini kupokelewa MOI akitokea Hospitali ya Taifa Muhimbili alionekana akiwa na jeraha chini ya bega la mkono wa kulia lililokuwa limeshondwa mbele na nyuma.
 Kufuatia hali hiyo madaktari wa taasisi hiyo walifanya uchunguzi na kushauri afanyiwe kipimo cha X-ray ili kubaini kama kuna mvunjiko kwenye sehemu ya jeraha na tathimini ilionyesha alikuwa na mvunjiko bila mifupa kupishana.
 
Pia imebainika kuwa jeraha alilopata halikuwa katika hali nzuri licha ya tiba ya mwanzo na kuamuliwa afanyiwe upasuaji mpya jambo ambalo limefanyika ili kuzuia maambukizi kama jeraha hilo lingeachwa hivyo hivyo.
 
Aidha Katibu huyo wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu nchini anaendelea na matibabu baada ya upasuaji huo.
 

No comments

Powered by Blogger.