Header Ads

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO AFUNGUA MAJADILIANO KUHUSU UTAFITI WA VYAMA VYA SIASA

 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifungua majadiliano. Katikati ni Mwenyekiti wa Majadiliano hayo kutoka Kituo cha Demokrasia na Maendeleo Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.

Mhe. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto afungua  Majadiliano kuhusu Utafiti wa Vyama vya Siasa na namna vinavyozingatia masuala ya Kisiasa katika Mtizamo wa Kijinsia nchini. Majadiliano hayo yameandaliwa  na Kituo cha Demokrasia na Maendeleo kwa Kushirikiana na Shirika la Kimataifa la IDEA. Aidha Utafiti kama huo umefanyika katika nchi 38 za Barani Afrika kutoka Vyama  mbalimbali 220 vya Siasa.
 Baadhi ya Washiriki wa Majadiliano hayo kutoka katika Vyama mbalimbali vya Kisiasa nchini wakifuatilia Taarifa ya Utafiti
 Mwakilishi wa Shririka la Kimataifa la IDEA Bibi. Rumbidzai Kandawasvika Nhundu akielezea sehemu ya taarifa ya Utafiti huo. Inaefutia ni Mhe.Ummy Mwalimu na Mhe.Agustine Lyatonga Mrema Mwenyekiti wa Majadiliano hayo
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar- es Salaam Dr. Bernadetha Kilian akiwasilisha taarifa ya Utafiti

No comments

Powered by Blogger.