Header Ads

MOYES SASA AINGIA MSITUNI KIKWELI KWELI...ATAKA SAINI YA KIFAA CHA BRAZIL

DAVID Moyes ameingia kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Brazil, Willian mwenye thamani pauni milioni 30.

Staa huyo wa Anzhi Makhachkala tayari amezivutia klabu za Liverpool na Tottenham Hotspur, lakini Manchester United wanaweza kuzipindua timu hizo.

Liverpool wanaendelea na mazungumzo na Anzhi kuhusiana na uhamisho wa Mbrazil huyo mwenye miaka 25 na wanauhakika kwamba watamnasa. Lakini sasa United wameingia kati na inasemekana 2Willian angependa kutua Old Trafford.
 
Target: Manchester United could hijack Liverpool and Tottenham's moves for Willian
Anatakiwa: Manchester United inaweza kuzipiga bao Liverpool na Tottenham kwa Willian
Under pressure: David Moyes wants to bring a big name to the club this summer
Tumbo joto: David Moyes anataka kusajili jina kubwa kabla ya dirisha kufungwa
Tottenham wameendelea kuvutiwa na staa huyo wa zamani wa Shakhtar Donetsk na wako tayari kumchukua kama Gareth Bale akikamilisha uhamisho wake kwenda Bernabeu.

Willian aliimbia ESPN kwamba yuko tayari kwenda Liverpool, alisema: “Kulikuwa na ofa ya Manchester City ambayo ilikataliwa. Sasa nasubiri ofa mpya siku zijazo kutoka kwa timu kadhaa, kama Liverpool. Kama Liverpool wakija, nji klabu kubwa. Natumaini ofa zitakuja na sina papara nasuburi kilichobora.

“Malengo yangu yako England. Naipenda Ligi Kuu ya nchini hiyo, nafurahia soka la Kiingereza na ni wazi kwamba hilo likitimia itakuwa poa sana, itakuwa nzuri sana kwangu na jina langu.”

United, wanaohaha kusaini staa mwenye jina kubwa wamepewa ofa ya kusajili kiungo mchezeshaji wa Real Madrid, Mesut Ozil kwa pauni milioni 40.

Staa huyo wa Ujerumani, 24, aliwahi kutakiwa na Sir Alex Ferguson baada ya Kombe la Dunia mwaka 2010, lakini akatua Real Madrid kwa pauni milioni 12.5. na sasa yuko tayari kuondoka Hispania.
Offer: Real Madrid are willing to sell Mesut Ozil to Man United for £40million
Ofa: Real Madrid wako radhi kumuuza Mesut Ozil kwenda Man United kwa pauni milioni 40

Wawakilishi wa Ozil wameshaweza wazi kwamba watakaribisha uhamisho kwenda United na Madrid wanaweza kukubali ofa ya pauni milioni 35 wakati huu wakisaka fedha za kumnasa Bale.

Staa huyo wa zamani wa Werder Bremen anamkataba na Madrid mpaka mwaka 2016, lakini anaonekana kuwa na hofu na kitendo cha Madrid kumsaka Bale kwa udi na uvuma mwaka mmoja baada ya kumsajili Luka Modric kutoka Spurs.

Moyes mwanzo alikuwa akitaka kiungo wa kazi na Modric alikuwa kwenye mawazo yake kama wakishindwa kumnasa Cesc Fabregas kutoka Barcelona.

Kocha huyo wa United amesisitiza kwamba atafanya usajili kabla ya dirisha kufungwa. Kwa sababu alikuwa anahitaji muda kidogo kuijua timu na aina ya wachezaji alionao na wale walio sokoni. 

Moyes pia anaweza kurudi kwa kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, lakini anajua kwamba Mbelgiji huyo hatakuwa jina kubwa kwenye usajili wa United.

Jana kocha wa Everton, Roberto Martinez aliionya United kwamba Fellaini hatapatikana kwa bei rahisi kama wanavyodhani. Moyes anatarajiwa kuweka ofa mezani ya kumsajili Fellaini, ambaye alimleta Everton kwa dau la uhamisho wa rekodi la klabu la pauni milioni 15 mwaka 2008.

Everton have not received an offer for Fellaini since the £23m buy-out clause in his deal lapsed on July 31 and it is thought United will offer less than £23m.

Kwa ishu ya Leighton Baines ilikuwa rahisi zaidi baada ya Everton kukataa ofa ya pauni milioni 12, United wakasema kwamba ndiyo ofa yao ya mwisho.
Going nowhere? Leighton Baines seems set to stay at Everton after United made a 'final' offer
Haendi kokote: Leighton Baines anaonekana kubaki Everton baada ya United kugoma kupanda dau.

No comments

Powered by Blogger.