Header Ads

MASHABIKI WA KANDANDA RAHA TUPU, ATN KURUSHA EPL NA BUNDESLIGA LIVE!!


IMG_0481 
Afisa Uhusiano wa Agape Associate Limited Bw. Brian Willium KULIA akiwaeleza waandishi mpando mpya wa kampuni hiyo yenye kituo cha Televisheni cha ATN kuanza kuonesha ligi kuu ya uiengereza(EPL) na Ujerumani(BUNDESLIGA) katika Msimu huu wa ligi KUSHOTO ni mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Vicent Tiganya.

PICHA NA ELIPHACE MARWA.

Na Hassan Silayo -MAELEZO.

Katika kuhakikisha inawapatia wapenzi wa soka nchini burudani ya mpira wa miguu kampuni ya Agape Associate Limited yenyekumiliki Kituo cha Televisheni cha ATN wanatarajia kuanza kuonesha ligi kuu za Uingereza(EPL) na ile ya Ujerumani(BUNDESLIGA).

Hayo yamesemwa leo na Afisa uhusiano wa kampuni hiyo Brian Willium katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Jijini Dar es Salaam.
“Kutokana na kuona mpira wa soka umekuwa na msisimko mkubwa nchini sisi kama Agape Associate Limited tumeamua kuonesha ligi mbili Maarufu duniani tukiwa na dhumuni kuongeza burudani kwa watanzania”Alisema Brian.

Pia Brian alisema mechi hizo zitakuwa zikioneshwa mara moja kwa wiki ikiwa ni kwa mechi za jumamosi na katika ratiba hiyo mechi za ligi kuu ya uingereza zitakuwa zikianza na kisha kufuatiwa na ligi kuu ya ujerumani.

1 comment

alone warrior said...

i liked your website, it has good design and nice collection of sports channels, but seems like your bundesliga live stream is not working, can you please fix it? anyways keep up the good work

Powered by Blogger.