Header Ads

MARTINO: SIMHITAJI LUIZ WALA AGGER, KLABU HAITASAJILI WACHEZAJI HAO WAWILI MAJIRA HAYA YA KIANGAZI!!

KOCHA mkuu wa Barcelona , Tata Martino amekanusha taarifa za kujihusisha na uhamisho wa wachezaji wawili wanaocheza ligi kuu soka nchini England, David Luiz au  Daniel Agger, na kuthibitisha kuwa anafurahia wachezaji wake wa safu ya ulinzi alionao kwa sasa katika  kikosi chake.
 
Wakatalunya wamekuwa wakihusishwa kutumia dau kubwa kuwasajili wachezaji hao wawili, ingawa klabu za Chelsea na Liverpool zimeonesha msimamo wa kutokuwauza.

Na kocha Martino katika mkutano na waandishi wa habari wakati akizungumzia mechi ya kwanza ya La Liga dhidi ya Levante amesema:m”Tunaye  Puyol, Pique, Mascherano, Bartra, hata Adriano.  Kama itatokea kutakuwa na majeruhi  dirisha dogo mwezi januari sio mbali”
Not needed: Barcelona were thought to be chasing a centre-back this summer, with David Luiz (above) and Daniel Agger top of the list 
Hahitajiki: Barcelona walikuwa wanahusishwa kuwafukuzia mabeki wa kati David Luiz (juu) kutoka Chelsea  na Daniel Agger (pichani Chini) wa Liverpool
Not needed: Barcelona were thought to be chasing a centre-back this summer, with David Luiz (above) and Daniel Agger top of the list 
Miambya hiyo ya soka la Hispania ilikumbwa na majeruhi katika safu yake ya ulinzi msimu uliopita na kugeuka kuwa uchochoro wa kupitisha magoli na walifungwa mabao 7-0 na Bayern Munich katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
 
Maneno ya kocha Martino yanamaanisha makocha  Brendan Rodgers na  Jose Mourinho  wanaweza kuendelea kuwamiliki wachezaji wao.

Rodgers amemteua  Agger kuwa nahodha msaidiz ili kumshawishi kubakia Anfield, wakati huo huo Mourinho kuhusu Luiz alisema “Tunataka abakie hapa na tunajua timu kubwa kama Barcelona inajaribu kumsajili beki wa kati bora zaidi duniani, lakini kwa kuwa wakweli, hakuna nafasi ya kumuuza David Luiz “.

  Gerardo Martino raia wa Argentina alirithi mikoba ya  Tito Vilanova 
Expectant: Tata Martino speaks to the media ahead of his first competitive game in charge of Barca 
Tata Martino ameanza kibarua kizito

No comments

Powered by Blogger.