Header Ads

Kibo Gold yaja tena na muonekano mpya

 Kampuni ya bia ya Serengeti leo imezindua  muonekano mpya wa bia inayosherehekewa sana mkoani hapa, Kibo Gold.   Uzinduzi huu uliofanyika katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Moshi, ulifikia kileleni kwa shughuli murua iliyoandaliwa na kampuni hii na kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja na wadau mbali mbali.    Bia hii ya Kibo sasa ina muonekano mpya wa chupa inayoashiria ubora wa kilichopo ndani.  Bia ni yenye ubora uleule wenye kiwango cha hali ya juu ila kwa chupa ya rangi ile ile iliyongarishwa na  shingo ndefu. Akiongea kwenye hafla hii Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi Mwiyombella alisema bia hii ya Kibo Gold imekuwa ikitambulika kwa ubora na ladha nzuri kwa wateja.   

“Kwa muonekano huu mpya wa chupa ya kisasa, tunaamini wateja wengi watavutiwa na kuipenda zaidi kwani ni muonekano unaokwenda na wakati.   Ubora wa bia hii, unakuwa dhahiri kweli kabisa ukizingatia kwamba inatengenezwa kwa maji yatiririkayo kutoka katika kilele cha juu kabisa cha mlima Kilimanjaro ambapo pia bia inazoa jina lake hili la ‘KIBO’, aliongeza Bi Nandi.


Kampuni ya bia Serengeti chini ya kampuni mama ya Diageo, inazingatia kanuni  na sheria zilizowekwa na kampuni hii kwenye ubora katika uzalishaji wa  bidhaa zote.  Muonekano wa bidhaa ni ule unaondena na soko za kimataifa na wa kuvutia.  Kampuni ya bia ya Serengeti  inatumia malighafi za kitanzania ili kuleta ubora halisi na vile vile kukuza uchumi wa Tanzania katika sekta ya kilimo.


Bia ya Kibo Gold ilirudishwa sokoni hapa Tanzania mwaka jana, 2012, mwezi wa sita baada ya kuwa haipo kwenye soko kadri ya miaka kumi.   Ni mojawapo ya bia zinazoongoza nyanda za kaskazini sasa hivi.  Bia hii inazalishwa katika kiwanda cha bia cha Serengeti cha Moshi na inasambazwa mkoani hapo na mikoa jirani, Arusha, Tanga, Manyara na Tanga kwa wingi.Tafadhali kunywa kistaarabu.  Haiuzwi kwa walio chini ya miaka 18.

Meneja miradi na uwajibikaji, Bi Nandi Mwiyombela akiongea mbele ya wasambazaji wa kinywaji cha Kibo Gold, katika hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho kipya jijini Moshi, Mwishoni mwa wiki iliyopita
Meneja wa kiwanda Cha Serengeti tawi la Moshi, Bw. Coleman Hanna, akiongea na wasambazaji wakubwa na waandishi wa habari katika hafla hiyo
 Hapa ni Meneja, na wasambazaji wake wakiinua bia juu kuashiria uzinduzi wa muonekano mpya wa Bia ya Kibo Gold
 Msambazaji wa kwanza kabisa wa bia za Serengeti mkoa wa Kilimanjaro Mama Kisela, akipokea bia ya Kibo Gold yenye muonekano mpya na ladha ileile  kutoka kwa Attu Mynah wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa wa bia hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda hicho mwishoni mwa wiki iliyopita.
Meneja Miradi endelevu na uwajibikaji lampuni  ya bia ya Serengeti  Nandi Mwiyombela (Katikati), Meneja wa kiwanda hicho Bw. Coleman Hanna wakionyesha mbele ya wasambazaji wa bia na waandishi wa habari aina mpya ya chupa yenye shingo ndefu ambayo bia ya Kibo Gold itapatikana kuanzia sasa, hafla hiyo ilifanyika katika kiwanda cha Serengeti Breweries kilichopo mjini Moshi.
Meneja wa kiwanda cha bia cha Serengeti cha mjini Moshi Bw. Coleman Hanna (katikati) akibadilishana mawazo na meneja mauzo wa kanda ya kaskazini Bw. Patrick Kisaka (kulia) wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa bia ya Kibo Gold uliofanyika kiwandani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments

Powered by Blogger.