Header Ads

HOSPITAL YA MKOA WA MOROGORO YAPIGWA JEKI NA KCB BENKI

Dkt.Haroun Nyagori ambaye ni bingwa wa Magonjwa ya moyo katika Hospital ya Mkoa wa Morogoro,akielezea umuhimu wa mashine ya Cardiac Monitor yenye thamani ya Tsh Milioni 12 mara baada ya kupokea msaada wa mashine hiyo toka kwa Meneja wa benki ya KCB tawi la Morogoro Bi.Hogla Laiser (katikati)
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt.Rita Lyamuya(kulia)akipokea msaada wa Mashine ya Cardiac Monitor kutoka kwa Meneja wa Benki ya KCB tawi la Morogoro Bi.Hogla Laiser.
Swaumu Hassani ambaye ni Mama mzazi wa Mtoto Ibrahim Salum akishuhudia mwanae akipatiwa vipimo kupitia mashine ya Cardiac Monitor na Dkt.Haroun Nyagori ambaye ni bingwa wa Magonjwa ya moyo katika hospital ya Mkoa wa Morogoro,Mashine hiyo yenye thamani ya shilingi Milioni 12 ilitolewa msaada na Benki ya KCB tawi la Morogoro hapo jana,anaeshuhudia kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Dkt.Rita Lyamuya.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na wafanyakazi wa Benki ya KCB tawi la Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano rasmi ya Mashine moja ya Cardiac Monitor iliyotolewa msaada na Benki hiyo hapo jana. 

No comments

Powered by Blogger.