Header Ads

HATARI KUBWA ARSENAL, WENGER AMEACHA WACHEZAJI 17 NA KASAJILI MMOJA TU NAYE PIA MAJERUHI

KITENDO cha kocha Arsene Wenger kutosajili majira haya ya joto kuna hatari kimatafuna mwenyewe, The Gunners ikionekana dhahiri kuelekea matatizoni.
Wakati wanafungua msimu na Aston Villa, The Gunners ina kazi kubwa kuhakikisha inapata kikosi cha kwanza cha wachezaji 11 na wakati huo huo benchi lake litakuwa na makinda zaidi.
 
Timu hiyo ya Kaskazini mwa London, imeacha wachezaji 17 huku yenyewe ikisajili mmoja tu na ambaye pia ni majeruhi.
Failed: Arsene Wenger has brought in only one player and released 17 this summer
Kufeli: Arsene Wenger amesaini mchezaji mmoja tu na kutema 17 majira haya ya joto
Reliant: Inactivity in the market will leave Arsenal relying on the likes of Nicklas Bendtner and Ryo Miyaichi this weekend
Wengine njiani kuondoka: Arsenal inaweza kufunga dirisha la usajili kwa kukuuza wawili zaidi Nicklas Bendtner na Ryo Miyaichi mwishoni mwa wiki hii

KIKOSI CHA KWANZA CHA SASA CHA ARSENAL

Makipa: Szczesny, Fabianski.
Mabeki: Mertesacker, Koscielny, Jenkinson, Gibbs, Vermaelen (inj), Monreal (inj), Sagna (inj).
Viungo: Rosicky, Oxlade-Chamberlain, Wilshere, Ramsey, Cazorla (travelled from Ecuador), Arteta (inj)Diaby (inj), Frimpong, Miyaichi.
Washambuliaji: Podolski, Giroud, Walcott, Sanogo (majeruhi), Park, Bendtner.
Kuna wasiwasi mkubwa na maswali mengi kuhusu kikosi cha kwanza cha timu hiyo, kwani 10 kati ya 24 waliomo kwenye orodha wanaonekana kabisa hawako tayari. 
Bacary Sagna alikuwa nje ya kikosi cha Ufaransa katikati ya wiki, Thomas Vermaelen, Abou Diaby na Nacho Monreal wote ni majeruhi wa muda mrefu, Mikel Arteta yuko nje pia wakati Santi Cazorla amesafiri Ecuador kucheza na Hispania. 
Aaron Ramsey pia alitemwa kikosi cha Wales huku mchezaji mpya pekee, Yaya Sanogo, mwenye umri wa miaka 20 tu, anaweza kukosekana mwanzoni mwa msimu kwa maumivu ya nyama.
Mchezaji huyo alitemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 21.

USAJILI WA THE GUNNERS MAJIRA HAYA YA JOTO... 

WALIOONDOKA: Andrey Arshavin (ametemwa), Denilson (Sao Paulo, bure), Sebastien Squillaci (ametemwa), Martin Angha (Nuremberg, dau siri), Craig Eastmond (Colchester, bure), Conor Henderson (ametemwa), Jernade Meade (Swansea, bure), Sanchez Watt (Colchester, bure), Johan Djourou (Hamburg, mkopo), Vito Mannone (Sunderland Pauni Milioni 2), Andre Santos (Flamengo, bure), Francis Coquelin (Freiburg, mkopo), Joel Campbell (Olympiacos, mkopo), Chuks Aneke (Crewe, mkopo), Marouane Chamakh (Crystal Palace, bure), Ignasi Miquel (Leicester, mkopo wa muda mrefu wa msimu), Gervinho (Roma, Pauni Milioni 8).
ALIYEINGIA: Yaya Sanogo (Auxerre, bure).
New boy: Yaya Sanogo is Wenger's only signing of the summer - and even he is injured
Mpya pekee: Yaya Sanogo ni mchezaji pekee aliyesajiliwa na Wenger majira haya ya joto na pia ni majeruhi
Well travelled: Santi Cazorla did a 10,000-mile round trip to play with Spain in Ecuador
Safari ndefu: Santi Cazorla alisafiri zaidi ya maili 10,000 kucheza na Hispania Ecuador

Bado wachezaji wengine wanne wa kikosi cha kwanza Arsenal- Emmanuel Frimpong, Ryo Miyaichi, Pak Chu-Young na Nicklas Bendtner wanachungulia mlango wa kutokea.
 
Frimpong alicheza mechi mbili tu alipokuwa akicheza kwa mkopo Fulham. Katika mkopo wa muda mrefu akiwa na timu iliyoshuka daraja, Wigan, Miyaichi alicheza mechi moja tu tangu mwanzo, huku mechi saba akitokea benchi. 
 
Park Chu-Young amecheza mechi 21 na kufunga mabao matatu akiwa Celta Vigo ambayo ilinusurika kwa pointi moja tu kushuka daraja hadi Segunda.
 
Na pia kuna Bendtner, Mdenmark ambaye amekuwa akicheza kwa mkopo kwa misimu miwili iliyopita naye anatarajiwa kuondoka.
 
Wenger amekuwa akihusishwa na kuwawania wachezaji kama Luis Suarez, Luiz Gustavo, Cesc Fabregas, Wayne Rooney, Bernard, Gonzalo Higuain, Adil Rami, Julio Cesar na Ashley Williams.
 
Super sub: Ryo Miyaichi will be another on the bench this weekend, but he only managed one start and seven substitute appearances at relegated Wigan
Super sub: Ryo Miyaichi anaweza kuanzia benchi mwishoni mwa wiki, lakini alicheza mechi moja tu alipokuwa kwa mkopo Wigan, huku saba akitokea benchi.
Concern: Thomas Vermaelen is one of a number of players with long-term injury troubles
Mashaka: Thomas Vermaelen ni mmoja kati ya majeruhi wa muda mrefu
Ready to step in? Arsenal's youngsters, including the highly-rated Chuba Akpom have conceded 12 goals to Colchester and Luton in the last two matches
Tayari kwa kazi? Miongoni mwa makinda wa Arsenal, ni Chuba Akpom anayepewa thamani kubwa, ambaye amefunga mabao 12 dhidi ya Colchester na Luton katika mechi mbili zilizopita

No comments

Powered by Blogger.