Header Ads

DALILI ZA KUTOSHA RONALDO KUREJEA MAN UNITED...MAKOCHA WAENDA KUMFUATILIA AKIICHEZEA URENO JANA

KLABU ya Manchester United inaendelea kumfuatilia Cristiano Ronaldo baada ya makocha Phil Neville na Steve Round kumshuhudia nyota huyo wa zamani wa Old Trafford akiichezea Ureno jana usiku.

Neville na Round walikuwa kwenye Uwanja wa Algarve kumshuhudia Ronaldo akifunga bao la jioni kuinusuru kuzama mbele ya Uholanzi kwa kupata sare ya 1-1 ya Robin van Persie.
 
United imetunza jezi namba saba (7)zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kuanza kwa msimu mpya kwa matumaini ya kutimiza ndoto za kumrejesha Ronaldo kutoka Real Madrid – miaka minne baada ya kutimkia Bernabeu kwa sau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 80.
 
Wanted man: Ronaldo scored the equaliser in Portugal's 1-1 draw with the Netherlands on Wednesday night
Anatakiwa: Ronaldo aliifungia bao la kusawazisha Ureno katika sare ya 1-1 na Uholanzi jana
Coaching team: David Moyes speaks to Neville and Round during Rio Ferdinand's testimonial on Friday
Jopo la makocha: David Moyes akizungumza na Neville na Round katika mchezo wa kumuaga Rio Ferdinand Ijumaa

Mustakabali wa mchezaji huyo umeendelea kuwa shakani Hispania, licha ya Rais wa Real, Florentino Perez kuhakikisha kwamba atasaini Mkataba mpya.
 
Na huku David Moyes na Mtendaji Mkuu mpya United, Ed Woodward wakiwa bado hawajasajili mchezaji yeyote tangu waanze kazi na tetesi zikizidi juu ya Wayne Rooney kuondoka, United inafahamu kwamba kumnasa Ronaldo watawapa mtikisiko wapinzani wao wote ndani na nje ya Uwanja.
 
Enlarge Eyeing up a return? Ronaldo winks at Arjen Robben before kick-off on Wednesday night
Anarudi? Ronaldo akisalimiana na Arjen Robben kabla ya mechi ya jana
Looking the part: Ronaldo touches up his hair before kick-off on Wednesday night
Ronaldo akirekebisha nywele zake jana
Winner: Ronaldo celebrates victory over FC Porto in the 2009 Champions League quarterfinal
Mshindi: Ronaldo akishangilia dhidi ya FC Porto katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2009
Antonio Valencia
Cristiano Ronaldo
Spesho Namba 7: Valencia amepokonywa jezi namba saba na sasa iko wazi baada ya kushindwa 'kuitendea haki' kama wachezaji waliomtangua

No comments

Powered by Blogger.