Header Ads

CHEKI JIMMY MASTER NA HEKA HEKA ZA UJIO MPYA WA DOBLE J FINAL


Jimmy Master

YULE muongozaji na mwigizaji Jimmy Mponda 'Jimmy Master' aliyetikisa  na mfululizo wa filamu za misuko iliyotoka sehemu ya kwanza hadi ya tatu na baadaye kujiongezea jina lingine akiitwa J Plus.
 
Kwa sasa nyota huyo amefunguka  kuwa yukombioni kutoa muvi ya mwisho inayoitwa Doble J Final  huku ujio huo ukiwa ni wa mwisho kutoka baada ya kutangulia  na Doble J sehemu ya kwanza na yapili zilizotoka mwaka jana.

"Mwaka jana nilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu hususani  wanaopagawa na filamu za mapigano na kujawa mambo ya  kipelelezi,"alisema J Plus.

Alisema Doble J Final pia ni ujio wake wa filamu nyingine ya mapigano na  kuna heka heka za kipelelezi ndani. J Plus aliyezoeleka sasa katika kuonesha ubabe wa kufa mtu , kwa sasa ujio wake huo unao tazamiwa kuingia sokoni mapema tu , mwezi ujao . 
 
Pia Jimmy Master amemshirikisha mbabe mwingine katika filamu za mapigano Ibrahim Mbwana  'Bad Boy' na pia wamo nyota wengine katika dulu la filamu kama Charles Magari , Hashim Kambi na Veronica Viankero.

No comments

Powered by Blogger.